Rafiki yangu mpendwa,
Huenda hili ni swali umekuwa unajiuliza kwa muda mrefu.
Unapoona wenzako ambao mmeanza kazi pamoja, kazi ambayo ni sawa na malipo yanalingana, ila wao wanapiga hatua huku wewe unabaki nyuma.
Au ni kwenye biashara ambapo unaona wengine wanaofanya biashara ya aina hiyo na mlioanzia kwa kiwango sawa wanapiga hatua wewe unabaki ulipo.
Watu wa kawaida, ambao hawawezi kufanikiwa huwa wanatafuta sababu za kuhalalisha hali zao.
Wanajiambia wale waliopiga hatua wamependelewa au wamepata bahati au kuna njia zisizo sahihi wanazotumia.
Ni kweli hivyo vinaweza kuchangia kwa namna fulani, lakini siyo sababu hasa.
Wale waliopiga hatua kuliko wewe kuna mambo mawili yanayowatofautisha na wewe ambayo kama hutayajua na kuyafanyia kazi, utaendelea kubaki hapo ulipo.
Jambo la kwanza ni namna wanavyofikiri.
Kuna watu wanapewa urithi na wanaweza kuuendeleza na kufanikiwa. Wakati kuna wengine wanapewa urithi na kuupoteza wote.
Kinachowatofautisha watu hau siyo wanachopewa, bali namna wanavyokichukulia.

Namna mtu anavyofikiri inaathiri sana yale anayofanya kwenye maisha yake. Wanaopiga hatua wanafikiri kwa uchanya, uwezekano na ukuaji.
Kwenye fikra zao wanaona picha kubwa ambayo wanapambana kuifikia. Wanaamini bila ya shaka yoyote kwamba watafikia picha hiyo.
Na pale wanapokutana na vikwazo mbalimbali, wanajua siyo mwishi wa safari, bali wanaimarishwa ili waweze kupokea makubwa.
Wasiofajikiwa wao hufikiri kwa udogo, uhasi na kutokuwezekana. Hawana picha kubwa, wanaona mengi ni mabaya na wanapokutana na changamoto wanaona ni mwisho.
Kama hutabadili namna unavyofikiri hutaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Jambo la pili ni namna watu wanavyofanya.
Kama watu wawili wanafanya kazi au biashara ya aina moja na mmoja akapiga hatua kuliko mwingine, ukimuangalia utaona wazi kuna vitu anafanya tofauti.

Wanaofanikiwa na kupiga hatua wanafanya mambo yao kwa namba ya tofauti kabisa.
Wana viwango walivyojiwekea katika kufanya, viwango ambavyo ni vya tofauti kabisa na wengine.
Wanakwenda hatua ya ziada na kutoa thamani kubwa tofauti na wanavyotegemewa kufanya.
Wanajua mafanikio ni mbio za muda mrefu na hivyo hujipanga vizuri kwenye ufanyaji wao.
Kamwe hawaahirishi yale waliyopanga kufanya, wana nidhamu kubwa ya kutekeleza kama walivyopanga.
Wale wasiofanikiwa huwa wanafanya mambo yao kwa mazoea, hawawezi kujituma wenyewe mpaka wasukumwe na ni wazuri sana kwenye kuahirisha yale waliyopanga kufanya.
Kama hutajifunza namna waliofanikiwa wanavyofanya na wewe kufanya kwa namna hiyo, utaendelea kubaki pale ulipo.
Habari njema kwako rafiki yangu ni una nafasi nzuri ya kujifunza kwa kina namna ya kufikiri na kutenda ili uweze kufanikiwa sana.
Kupitia kitabu kipya cha TABIA ZA KITAJIRI, unakwenda kujifunza tabia ulizonazo sasa unazopaswa kuzivunja na tabia mpya unazopaswa kujijengea ili kufanikiwa.
Kitabu hiki kinapatikana kwenye app ya SOMA VITABU ambayo ipo kwenye Play Store.
Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi (10,000/=) lakini leo nakupa kama zawadi kwa kuchangia kiasi kidogo cha tsh elfu moja (1,000/=) ili kukipata.
Lengo langu ni kila mtu akisome kitabu hiki, ayapate maarifa haya na kuweza kuyabadili maisha yake.
Chukua hatua sasa ya kuipata zawadi hii ya kipekee sana niliyokupa.
Fungua sasa http://www.bit.ly/somavitabuapp kukipata kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI.
Kama hutumii simu ya android na unapenda kukipata kitabu hiki kwa njia ya email, tuma ujumbe wasap namba 0717 396 253. Ila zawadi ipo kwenye app tu, kupata kitabu kwa njia nyingine unalipia bei yake halisi.
Badili namna unavyofikiri na namna unavyotenda na utaweza kuyabadili maisha yako na kupiga hatua kubwa. Soma sasa kitabu cha TABIA ZA KITAJIRI.
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.