Watu wengi hudhani kutangaza biashara ndiyo kufanya masoko. Matangazo ni sehemu ya masoko ila siyo sehemu pekee.

Masoko ni mfumo wa kuifanya biashara ijulikane na wateja, washawishike kununua na waendelee kuiamini biashara hata baada ya kununua.

Masoko yanahusisha kila eneo la biashara kuanzia kwenye kuandaa bidhaa au huduma, kutengeneza hadithi ambayo wateja wanaielewa na kuiamini na kuwashawishi watu kununua.

Masoko yakifanywa kwa mkakati mzuri, biashara inanufaika sana, kwa kupata wateja wengi, kukuza mauzo na kuongeza faida. Weka nguvu za kutosha kwenye masoko ili biashara yako iweze kufanya vizuri.

Hapa kuna hatua tano muhimu za kuzingatia kwenye masoko, zijue na uzizingatie; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/15/2327

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma