Watu wengi huwa wanalalamikia kipato wanachoingiza, wakisema ni kidogo sana na siyo sahihi kwao. Wanaona wanastahili kulipwa zaidi ya hapo.

Kwenye uchumi wa soko huria, unastahili kile unacholipwa, hata kama ni kidogo kiasi gani, kwa sababu kinaendana na thamani unayozalisha.

Hivyo kama unataka kulipwa zaidi, wajibu wako ni mmoja, zalisha thamani kubwa zaidi. Hulipwi kwa muda unaofanya kazi wala kwa elimu yako, bali unalipwa kulingana na thamani unayopeleka kwenye soko.

Kama unalipwa kidogo, thamani unayotoa ni ndogo. Ukiongeza thamani unayotoa utaweza kulipwa zaidi.

Ukurasa wa kusoma ni kanuni ya kipato ambayo ina vitu vinne muhimu vya kuzingatia; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/17/2329

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma