Kila anayefikia mafanikio makubwa kwenye maisha, huwa kuna bahati anakutana nazo kwenye safari yake ya mafanikio.

Lakini bahati hizi haziendi kwa aliyelala, bali zinaenda kwa aliye kwenye mapambano.

Kwa kuwa hujui lini bahati itakufikia, wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha uko hai na uko kwenye mapambano ili bahati inapokuja ikukute.

Ukikata tamaa na kuachana na mapambano ya mafanikio, unakuwa umeondoa nafasi za kukutana na bahati.

Ukiwa haupo hai pia huwezi kukutana na bahati. Hivyo epuka kuingia kwenye hatari zitakazokuwa kikwazo kwako kukutana na bahati nzuri.

Ukurasa wa kusoma ni hatua za kupata chochote unachotaka; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/20/2332

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma