Rafiki yangu mpendwa,
Ukweli unapaswa kusemwa  na kupokelewa kama mtu anataka kupiga hatua.
Na ukweli kuhusu mafanikio ni huu, huwezi kufanikiwa kwa kuendelea kubaki hapo ulipo, ukifanya unachofanya na kwa namna uliyozoea kufanya.

Ni Albert Einstein aliyewahi kusema ujinga ni kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile na kutegemea matokeo tofauti.
Kauli hiyo ni kweli pia kwenye mafanikio, huwezi kuendelea kufanya unayofanya na kwa namna unavyoyafanya halafu ufanikiwe, ni kujidanganya huko.

Mafanikio pia yanaendana sana na kauli maarufu inayosema kila mtu anataka kwenda mbinguni, lakini hakuna anayetaka kufa.
Mafanikio ni kama mbingu ambayo kila mtu anaitaka, lakini kuyafikia lazima upitie kifo, lazima ufe kwa namna ulivyo sasa na uzaliwe upya ndiyo uweze kufanikiwa.

Kama unabisha hili siwezi kukulaumu, ni kwa sababu hujafanikiwa na hayo ni matokeo ya kukataa kufa ulivyo sasa ili uweze kuzaliwa upya.
Unachoweza kufanya hapo ulipo ni kuchagua mtu yeyote aliyefanikiwa na kuangalia maisha yake kisha kuyalinganisha na ya wengine.

Utajionea wazi kwamba kuna tofauti kubwa sana kwa namna waliofanikiwa wanaishi maisha yao na kufanya mambo yao ukilinganisha na wale ambao hawajafanikiwa.
Kwa wasioelewa hudhani hao waliofanikiwa wanaishi hivyo kwa sababu ndiyo miiko waliyopewa na waganga wao wa mafanikio.

Sasa leo nataka niwe mganga wako wa mafanikio na kama unataka kufanikiwa kweli, kuna vitu unapaswa kuvijua na kuvifanyia kazi mara moja bila kuendelea kupoteza muda.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA kuna dhana tunaita UBATIZO WA MAFANIKIO. Kama ambavyo unajua au umekuwa unasikia, kuna dini huwa zinafanya ubatizo kwa waumini wao.
Ubatizo huo ni alama ya mtu kuachana na maisha ya zamani na kuanza maisha mapya ya imani.
Ubatizo ni tukio muhimu sana kiroho, unamuua mtu wa zamani na kuzaa mtu mpya.

Kwenye mafanikio pia unapaswa kufa uliye sasa na uzaliwe uliye mpya ili uweze kufanya makubwa na ya tofauti.

Dhana hii ya KISIMA CHA MAARIFA ni pana na utajifunza kwa kina ukiwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ila hapa kuna mambo manne napenda uyajue kama unataka mafanikio makubwa.

Moja; Nenda Nyikani.

Kuna mabadiliko makubwa mno ya kimtazamo na kiimani unayopaswa kufanya kama unataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Hapo ulipo sasa ni matokeo ya imani na mitazamo ambayo umekuwa nayo huko nyuma.
Kama hutanadili hayo mawili, haijalishi kipi kitatokea nje, hutaweza kufanikiwa.

Chukua mfano wa wanaoshinda bahati nasibu, ambao wanapata fedha nyingi, nini kinatokea baadaye? Wanapoteza zote.
Chukua pia mfano wa wanaopata mafao au mirathi, wanapata fedha au mali nyingi kwa wakati mmoja, wanaishia kupoteza zote.

Kinachotokea ni watu hao wanakuwa wamebadilika nje, lakini ndani wamebaki walivyokuwa.
Sasa kwa kuwa ndani ndiyo kuwatawala nje, ndani ya muda mfupi watu hao wanakuwa wamerudi kwenye hali ya mwanzo.

Hatua ya kwanza na muhimu kabisa kwenye kufanikiwa ni kwenda nyikani, ili kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako.
Dhana hii ipo kwa kina kabisa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Mbili; Toa Kafara.

Bila kutoa kafara, huwezi kufanikiwa.
Kutoa kafara ni kuamua kuachana na vitu unavyovipenda sana kwa sasa lakini ni kikwazo kwako kufanikiwa.

Chochote kinachochukua muda, nguvu na umakini wako kwa sasa lakini hakichangii wewe kufanikiwa zaidi ni kikwazo kwako.

Tunaita kutoa kafara kwa sababu siyo kitu kinachofurahisha.
Itakuuma sana kuachana na vitu unavyovipenda.
Utajisikia vibaya kutengana na watu uliowazoea sana.
Utaona kama kuna kitu unakosa pale utakapoachana na anasa zote ulizozoea sasa.

Lakini hakuna namna, kama unataka kupata ambacho hujawahi kupata, lazima uwe tayari kupoteza kile ulichonacho sasa.
Kama una kikombe kimoja ambacho kimejaa chai, lakini kuna naziwa pia, lazima umwage chai ili uweze kuweka maziwa.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kuzijua kafara unazopaswa kutoa mara moja ili uache kuwa kikwazo kwa mafanikio yako mwenyewe.

Tatu; Jipe Masharti.

Kwa asili sisi binadamu ni wavivu, tunapenda vitu rahisi na visivyotuumiza.
Lakini hakuna mafanikio yanayotokana na vitu rahisi na visivyoumiza.
Hivyo kama utataka mwili wako na hisia zako vikuendeshe vinavyotaka, hutaweza kufanikiwa.

Lazima ujipe masharti ambayo utayafuata kila siku bila kuacha. Masharti hayo yanakuwa ndiyo msaafu wa maisha yako.
Lazima uyatimize kama ulivyopanga bila ya kujali unajisikia au hujisikii.
Haijalishi nini kinakuwa kinaendelea kwenye maisha yako, wewe unasimamia masharti yako.

Kulingana na maisha yako na mafanikio unayotaka kufikia, yapo masharti unayopaswa kujiwekea. Kwenye KISIMA CHA MAARIFA utaweza kujua masharti ambayo wewe unapaswa kujiwekea.

Nne; Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Safari ya mafanikio ni ngumu, ina vikwazo na changamoto nyingi.
Utakapoamua kubadilika wanaokuzunguka hawatakuachs kirahisi.
Utakapotoa kafara utatamani kurudi kwenye maisha ya zamani.
Utakapojiwekea masharti kuna vishawishi vitakuja kwako kutaka uyavunje.
Na katika safari utakutana na magumu na hata kukaribia kukata tamaa.

Ukiwa peke yako kwenye hii safari, ni rahisi sana kukata tamaa.
Hivyo unapaswa kuwa sehemu sahihi, ambapo unapata miongozo sahihi na kushirikiana na watu sahihi.
Sehemu hiyo ni KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni huduma ya mafunzo na ukocha ambayo nimekuwa naitoa kwa wale ambao wana kiu ya kufika kwenye mafanikio makubwa.
Huduma hii ina watu wengi sahihi kwako kushirikiana nao ili uweze kufanikiwa.
Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA unapata mafunzo na mwongozo sahihi wa kocha ili uweze kufanikiwa.

Nafasi ya kipekee kwako.

Kwa muda sasa nimekuwa sipokei wanachama wapya kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa sababu nimeweka nguvu kufanya kazi na wanachama waliopo sasa.

Lakini hili ni juma la kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu, ambapo huwa nina utaratibu wa kuyatafakari maisha yangu kwa kuangalia nilikotoka, nilipo sasa na ninakotaka kufika.

Katika juma hili natoa nafasi za kipekee kwa wanaopenda kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili waweze kufika kwenye mafanikio makubwa.
Kwa watakaojiunga kwenye mwezi huu wa Mei, nitawapa nafasi ya kuwa na mazungumzo ya simu ambapo tutakwenda hatua kwa hatua kujua mabadiliko ya kufanya kwenye maisha yako, ili wewe uende kutekeleza tu.

Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA, upate mafunzo na mwongozo sahihi kwa mafanikio yako.
Ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA ni tsh laki tatu (300,000/=)
Kujiunga tuma ujumbe kwa wasap kwenda namba 0717 396 253 ujumbe uwe na maneno KISIMA CHA MAARIFA.

Nafasi ya mazungumzo ya kujua hatua za mtu kuchukua kwenye maisha pia ipo wazi kwa wanachama waliopo kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Kama tayari ni mwanachama na ungependa tuwe na mazungumzo hayo, nitumie ujumbe kwa wasap namba 0717 396 253.

Kila mtu anapenda mafanikio makubwa, lakini ni wachache tu ambao wanayafikia.
Wewe unaweza kuwa mmoja wa wachache hao kama utakuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Karibu sana twende pamoja kwenye safari hii.

Rafiki yako anayekupenda sana
Kocha Dr Makirita Amani.