Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia mtandao wa intaneti.

Mtandao wa intaneti umeleta mapinduzi makubwa duniani, umerahisisha kila kitu ikiwepo kuingiza kipato.

Hapa kuna mawazo kumi unayoweza kutumia kuingiza kipato kwa kutumia mtandao wa intaneti mara moja.

  1. Anzisha blog ambayo utaweka maudhui mbalimbali na kisha kuitumia kuweka matangazo au kuuza bidhaa na huduma zako mwenyewe.

  2. Anzisha channel ya YouTube ambapo utaweka maudhui, kujenga wafuasi na kisha kuweka matangazo au kuuza bidhaa na huduma zako mwenyewe.

  3. Tengeneza kurasa za mitandao ya kijamii, kuza wafuasi na zitumie kutangaza biashara za wengine au biashara zako mwenyewe.

  4. Kuwa mshauri wa kile ambacho una ujuzi au uzoefu mkubwa nacho kupitia mtandao wa intaneti.

  5. Uza ujuzi wako kwenye tovuti mbalimbali ambapo watu hutafuta watu wa kuwafanyia kazi mbalimbali. Kama ubunifu wa picha na mengine. Mfano mtandao wa Freelancer.

  6. Watengenezee wengine blogu na tovuti na wakulipe.

  7. Wauzie wengine majina ya tovuti (domain name) au mahali pa kuhifadhi tovuti zao (hosting) kwa gharama nafuu. Wewe unanunua nafasi kubwa kisha kuwagawia wengine.

  8. Andika vitabu na uza kama nakala tete kupitia njia mbalimbali.

  9. Kuwa mwenye ushawishi mitandaoni (influencer) na tumia ushawishi huo kuwa balozi wa kampuni mbalimbali.

  10. Andaa kozi ya kile ulichosomea au una uzoefu nacho na kisha uza mtandaoni.

Nyongeza; uza chochote ulichonacho kupitia mtandao wa intaneti, jijengee ushawishi mkubwa na uza.

Kila wazo hapo linafanya kazi, ila kazi na muda vinahitajika.
Kama una mtandao wa intaneti, usiishie tu kununua mabando, utumie pia kuingiza kipato.
Ukichagua wazo lolote hapo au jingine lolote, karibu tushauriane juu ya utekelezaji wake.

Kocha.