Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia blogu.
Blogu ni kitu ambacho kila mtu anaweza kuanzisha na kuendesha kama una msukumo mkubwa ndani yako wa kushirikisha kile unachojua, unachojifunza au ulicho na uzoefu nacho.
Hapa kuna mawazo kumi ya kuingiza kipato kwa kutumia blogu.
- Kuweka matangazo ya adsense, hapa unaunganisha blog yako kwenye mfumo wa matangazo wa Google kisha wao wanaweka matangazo na watu wanapoyabonyeza unalipwa.
-
Kuweka matangazo ya biashara zako mwenyewe unazofanya.
-
Kuweka matangazo ya biashara za watu wengine.
-
Kuuza vitabu kwa nakala tete na ngumu.
-
Kuandaa kozi na kuuza kupitia blog.
-
Kuwa na makala za kulipia ambapo ili mtu azisome anapaswa kulipia.
-
Kuanzisha, kukuza na kuuza blog kwa wengine.
-
Kushauri watu kwa malipo wanaokutafuta kupitia blog.
-
Kuwa affiliate kwa kuuza bidhaa za wengine kupitia blog yako na kulipwa kamisheni. Mfano unaposhauri watu wasome kitabu fulani, ukiwa affiliate wa Amazon na ukaweka link na mtu akakinunua kupitia link hiyo, wewe unalipwa kamisheni.
-
Kuwasaidia wengine kuanzisha na kukuza blog zao. Kama umeweza kuanzisha blog yako na kuikuza mpaka kufikia kuingiza kipato, unaweza kuwasaidia wengine nao kufanya hivyo.
Mawazo haya yanafanya kazi na yanatumiwa na wengi, ila unahitaji kuweka kazi na muda mpaka wazo liweze kuleta manufaa.
Kama utachagua kufanyia kazi wazo lolote, karibu tushauriane namna bora ya kulitekeleza.
Kocha.
Kocha kuna affliate membership ya SOMA VITABU TANZANIA
LikeLike
Bado hatujawa nayo, lakini ndiyo mpango pale app itakapokaa sawa.
LikeLike