Umekuwa unahangaika sana kutafuta ushauri kwa watu wasiojua chochote kuhusu wewe na unachofanya, wakati yupo anayekujua vizuri na kuweza kukushauri vyema kabisa.Sauti iliyo ndani yako ni mshauri mzuri kwako, sauti hiyo inakujua wewe tangu unazaliwa, inakumbuka kila ambacho umewahi kupitia na inajua nini kizuri kwako.Sauti hiyo imekuwa inajaribu kuwasiliana na wewe ila umekuwa unaipuuza. Unapaswa kuwa na utulivu mkubwa ili uweze kuisikia na kuielewa sauti ya ndani yako.Hivyo pangilia siku yako kwa namna ambayo unapata muda wa kuwa na utulivu ili uisikilize sauti ya ndani yako kwenye yale muhimu inakushauri.Ukurasa wa kusoma ni mlango wa sita wa fahamu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/27/2339#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma