Kila mmoja wetu ana ndoto kubwa sana anazotamani kuziishi kwenye maisha yake. Lakini wengi hawaishi ndoto zao, huku wakijipa visingizio mbalimbali wakati sababu ya kweli ni moja, wanakosa ujasiri wa kuziishi ndoto hizo.

Kwa kuwa kuishi ndoto kunakutaka uwe wa tofauti, bila ujasiri hutaliweza hilo. Ujasiri unatokana na kujua unachotaka, kujiamini na kuwa na maarifa ya kutosha.

Hakuna anayeweza kukupa ujasiri, ni kitu unapaswa kujijengea mwenyewe. Jijengee ujasiri ili uweze kuziishi ndoto zako.

Ukurasa wa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/29/2341

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma