Kusoma ni nguvu ya miujiza inayoweza kuyabadili sana maisha yako. Kusoma kunakujengea mtazamo sahihi, kunaimarisha uwezo wako wa kufikiri na kufanya maamuzi na kukupa utulivu mkubwa.

Kusoma pia kunaiwezesha akili yako kusafiri kwenda maeneo mbalimbali na nyakati mbalimbali hivyo kukupa uzoefu mbalimbali.

Kumbuka kauli inayosema wapumbavu huwa hawajifunzi, wajinga hujifunza kwa makosa yao na werevu hujifunza kwa makosa ya wengine. Huna muda wa kujaribu kila kitu ndiyo ujifunze, badala yake soma ili ujifunze kupitia makosa ha wengine.

Ukurasa wa kusoma ni muujiza unaohitaji kutumia; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/05/30/2342

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma