2345; Mageuzi ya teknolojia yamepiku mageuzi ya akili…
Tunachokiona kwenye maisha ya sasa, hasa zama hizi za mitandao ya kijamii, ni mageuzi ya teknolojia kwenda kasi kuliko mageuzi ya akili.
Kwa mamilioni ya miaka, binadamu tulikuwa tunaishi kwenye makundi madogo madogo ya watu wasiozidi 30. Hiyo ilikuwa rahisi kumjua kila mtu ndani ya kundi na kumwamini pia.
Baadaye makundi yakawa yanakua na idadi ya watu ambao mtu aliweza kuwafahamu ikafikia 150. Kwenye kundi la watu 150, hata kama humjui mtu moja kwa moja, unamjua anayemjua na hilo kurahisisha ufanyaji wako wa maamuzi kuhusu mtu yeyote.
Sasa ghafla tumejikuta kwenye hali ambayo tumeunganika na maelfu ya watu, ambao wengi hatuwajui moja kwa moja na pia hatumjui anayemjua mwingine moja kwa moja.
Mbaya zaidi ni pale maelfu hao wa watu unaojuana nao mtandaoni wanapokushirikisha matatizo yao mbalimbali na kutaka uyajali kama wanavyoyajali wao.
Kama hiyo haitoshi, maelfu hao wa watu unaojuana nao mtandaoni, wanaishi maisha ya kuigiza. Hakuna hata mmoja anayeishi maisha halisi kwako.
Pamoja na wewe kujua hilo, bado unajikuta ukijilinganisha na watu hao na kuona wana maisha mazuri kuliko wewe.
Siyo kweli kwamba watu unaowaona kwenye mitandao ya kijamii wana maisha mazuri kuliko wao. Ni vile tu unajijua wewe mwenyewe kuliko unavyowajua wao. Ungepewa siku moja ya kuishi kwenye maisha yao, ungeshukuru sana kwa maisha uliyonayo sasa.
Hii ni kusema, kufuatilia watu kwenye mitandao ya kijamii kunakuchosha na hakuna manufaa yoyote unayoyapata.
Unahangaika na watu usiowajua na wasiokujua,
Wanakulazimisha ujali mambo wanayojali wao ambayo hayana tija kwako,
Na unatamani ungekuwa na maisha kama yao wakati ni waigizaji tu.
Hakuna cha kulaumu hapa, wewe jua teknolojia imekua kwa haraka kuliko ukuaji wa ubongo wako na usiruhusu teknolojia ikusumbue.
Kocha.
Asante Sana kocha.
LikeLike