Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia pikipiki.

Kila mtu anapofikiria kuingiza kipato kwa pikipiki anafikiria njia moja iliyozoeleka ambayo ni bodaboda.

Hilo limepelekea bodaboda kuwa nyingi mitaani na ushindani kuwa mkali.

Kuna njia nyingine nyingi za kuingiza kipato kwa kutumia pikipiki.
Hapa ni 10 katika njia hizo.

  1. Njia iliyo maarufu ya bodaboda.

  2. Kujiunga na teknolojia za usafirishaji ambazo zinaandikisha pikipiki pia.

  3. Kufanya biashara ya kutumwa na watu kwenda kuwachukulia mahitaji mbalimbali.

  4. Kufanya biashara ya kusambaza vifurushi vidogo vidogo.

  5. Kukodisha pikipiki kwa watu wanaotaka kutumia kwa siku chache.

  6. Kuwa na mkataba na abiria ambao wanabebwa na kulipa kwa muda mrefu kwa bei ya punguzo.

  7. Kutumia kubeba mizigo ya wastani kwenye eneo ambalo usafiri ni shida.

  8. Kuendesha mfumo mzuri wa usimamizi wa pikipiki za wengine.

  9. Kutumia pikipiki kama dhamana ya kupata fedha au chombo kingine.

  10. Kununua pikipiki kutoka kwa watu, kuzirekebisha na kuziuza kwa wengine.

Badala ya kuangalia pikipiki kwa fursa ya bodaboda pekee, angalia na fursa hizo mbadala ili kuweza kuingiza kipato zaidi.

Kocha.