2353; Unaweza Kutabiri Kwa Haya Matano…

Unaweza kutabiri iwapo biashara mpya itafanikiwa au kushindwa kwa kuangalia maeneo haya matano.

Moja ni wazo, je wazo ni sahihi kwa mwanzilishi wa biashara. Kila wazo ni zuri, lakini inategemea sana nani anatekeleza wazo hilo.
Kama mtekelezaji hana hamasa na msukumo mkubwa kwenye wazo lake, itakuwa vigumu kufanikiwa.

Mbili ni timu, mafanikio ya aina yoyote yale ni matokeo ya timu inayofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Kwa kuona jinsi timu inavyofanya kazi unaweza kujua ni matokeo gani yatakayopatikana.

Tatu ni muda, kuna muda sahihi na usio sahihi kwa wazo lolote lile. Wazo likishakuwa limeeleweka na kila mtu, tayari umeshachelewa. Ukishasikia watu wanaimba fursa kwenye jambo fulani, umeshaikosa.

Nne ni fedha, upatikanaji wa fedha za kutosha ni kigezo muhimu cha kufanikiwa au kushindwa kwa biashara.

Mfumo mzima wa biashara. Thamani kuu inayozalishwa ni ipi, inawafikiaje watu na wanalipiaje ni eneo muhimu. Je biashara inauza kwa biashara nyingine au moja kwa moja kwa wateja?

Kwa kuangalia maeneo hayo matano, utaweza kupata picha kama biashara itafanikiwa au kushindwa.
Na matatu ya mwanzo, yaani wazo, timu na muda ni muhimu zaidi.

Kocha.