
Ukishajiwekea lengo, kinachofuata ni wewe kupambana mpaka ulifikie lengo hilo. Usipoteze nguvu zako kwenye kujishawishi kulibadili lengo kwa sababu unaona huwezi kulifikia.
Badili mikakati na njia unazotumia, lakini usibadili lengo. Hata kama huoni namna ya kulifikia lengo, wewe amini kwenye lengo lako na kaa kwenye mchakato.
Tathmini kila hatua unazochukua na kuona kama ni sahihi na uendelee nazo au unapaswa kuziboresha.
Pambana na malengo unayojiwekea mpaka uyafikie.
Ukurasa wa kusoma ni kung’ang’ana na lengo, siyo njia; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/11/2354
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma