Kuna mambo mengi umewahi kujifunza kwenye maisha yako na kujiambia siku moja utayatumia, lakini umeshayasahau kabisa.Kuna mawazo mazuri yamewahi kukujia na ukajiambia utakuja kuyafanyia kazi ila umeyasahau kabisa.Kama hutatumia mawazo au maarifa unayoyapata wakati bado ni ya moto kabisa, nafasi ya kuyapoteza ni kubwa.Kila unapojifunza kitu, jiulize hapo hapo unawezaje kukitumia kwenye maisha yako na kisha chukua hatua mara moja.Unapoweka kwenye matendo kile unachojifunza, unakifanya kuwa sehemu yako na hutakisahau haraka.Kila unapojifunza kitu au kupata wazo jipya, jikumbushe kama hutatumia mara moja basi utakipoteza.Ukurasa wa kusoma ni kutumia kabla hayajapoa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/13/2356#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
#TAFAKARI YA LEO; TUMIA AU POTEZA…