
Hakuna kitu chenye gharama kubwa kwako kama usumbufu unaokuzunguka.
Huwezi kuona gharama hiyo haraka kwa sababu akili yako inapata raha kirahisi.
Ni baada ya muda mrefu ndiyo unakuja kugundua umekuwa unafanya kazi za kawaida na zisizo na ubunifu.
Kutaka kwako kujua kila kinachoendelea kumepunguza umakini wako kwenye yale unayofanya na umeishia kuyafanya kwa viwango vya chini mno.
Anza sasa kulinda umakini wako na kuutumia vizuri. Ondokana na usumbufu na weka umakini wako wote kwenye kile unachochagua kufanya ili uweze kukifanya kwa ubora na ubunifu mkubwa.
Ukurasa wa kusoma ni kujipa zawadi ya ubunifu; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/16/2359
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma