
Ipo kauli ya kiswahili inayosema wengi wape, kauli hiyo ni sahihi kwenye mambo ya kawaida.
Inapokuja kwenye mafanikio makubwa, wengi huwa hawapo sahihi. Kwa sababu njia ya kuelekea kwenye mafanikio ni ngumu na yenye vikwazo na changamoto nyingi, wengi huwa wanaikwepa.
Hivyo ukikutana na kitu ambacho wengi wanakikubali na kukisifia, jua siyo kitu kinachoweza kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Wengi wanapenda vitu rahisi, vitu walivyozoea kufanya na hawataki kabisa kujaribu vitu vipya ambapo wanaweza kukutana na magumu na wakashindwa.
Popote palipo na wengi, ni mahali ambapo mafanikio makubwa hayawezi kupatikana. Hivyo kuwa makini sana na vitu unavyojihusisha navyo, unaweza kujizuia usifanikiwe wewe mwenyewe.
Ukurasa wa kusoma ni ingekuwa rahisi kila mtu angefanya; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/06/22/2365
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma