Vyote viwili haviwezi kwenda pamoja. Ukitaka ueleweke na kila mtu huwezi kufanikiwa. Na ukitaka upate mafanikio makubwa, huwezi kueleweka na kila mtu.

Wanaofikia mafanikio makubwa wanajali zaidi ndoto zao kuliko wengine wanawachukuliaje. Wanaoshindwa wanajali sana wengine wanawachukuliaje kuliko wanavyojali ndoto zao kubwa.

Kipenga kimepulizwa, unachagua upande upi? Ukichagua upande wa kuridhisha watu safari yako haitakuwa ngumu, ila pia haitakupa matokeo makubwa.

Ukichagua upande wa ndoto yako inabidi uwe na ngozi ngumu kweli kweli, maana kila mtu atajatibu kuikata ngozi yako. Ni kuamua kulipa gharama sasa au baadaye.

Ukurasa wa kusoma ni kuangalia walikotoka na siyo walipo sasa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/07/2380

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma