Mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara.

Mauzo ndiyo injini ya biashara yoyote ile. Bila mauzo hakuna fedha inayoingia kwenye biashara na hapo hakuna biashara.

Kila biashara inaweza kuongeza mauzo zaidi ya inavyofanya sasa, hata kama mauzo yako juu kiasi gani.

Hapa ni mawazo 10 ya kuongeza mauzo kwenye biashara yoyote ile.

  1. Kutafuta wateja wapya na kuwashawishi kununua.

  2. Kuuza bidhaa au huduma mpya kwa wateja wa zamani.

  3. Kuwauzia wateja bidhaa zinazoendana kwa pamoja.

  4. Kuwashawishi wateja kununua kwa kiwango kikubwa kwa kuweka ofa.

  5. Ongeza watu wa mauzo zaidi.

  6. Kuzidisha mawasiliano wa wateja ambao walishanunua.

  7. Kuongeza juhudi za masoko.

  8. Kuchukua maoni ya wateja na kuyafanyia kazi.

  9. Kutoa ofa kipindi ambacho wateja wako kwenye manunuzi makubwa.

  10. Kuwashawishi wateja kuleta watu wengine na kisha kupata kamisheni.

Kwa njia hizi 10, unaweza kuuza zaidi ya unavyouza sasa na biashara yako ikanufaika sana.
Anza kuzifanyia kazi na kama umeshaanza ziboreshe zaidi.

Kocha.