2390; Kipi Kibaya Zaidi Kinaweza Kutokea?

Unapoweka mipango yako, huwa unaangalia mambo yakienda vizuri tu.
Kama ni biashara, unangalia upande wa faida tu.
Kama ni tabia unajijengea, unaangalia manufaa yake tu.

Tunapenda sana mambo yaende vizuri, lakini hilo liko nje ya uwezo wetu.
Kitu pekee tunachoweza kudhibiti ni juhudi unazoweka na siyo matokeo unayopata.

Hivyo kwa kila mipango unayoweka, jiulize pia ni kipi kibaya zaidi kinachoweza kutokea.
Lengo la swali hilo siyo kuathiri matokeo, bali kujiandaa na yale yanayoweza kutokea, ambayo hupendi yatokee.

Lengo ni kujiandaa kwa mabaya yanayoweza kutokea kabla hata hayajatokea. Ili yanapotokea usishangae, badala yake uwe tayari umejiandaa.

Kingine pia ni kuangalia kama kweli unaweza kuvuka magumu unayoweza kukutana nayo.
Wengi huangalia mazuri tu na wanapokutana na mabaya wanakata tamaa.
Unapoona uwezekano wa matokeo hayo mapema, unaamua kama kweli upo tayari kuendelea au bora ufanye kingine unachoweza kuvumilia.

Unapochagua cha kufanya, usiangalie tu manufaa au faida unayopata, bali pia angalia changamoto na magumu unayoweza kukutana nayo na uone kama unaweza kuyavumilia.

Kocha.