Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kutumia fedha.
Fedha ni mbegu, ambayo ukiipanda fedha inazaa fedha zaidi.
Na njia ya uhakika ya kufika kwenye utajiri na uhuru wa kifedha ni kutumia fedha kuzalisha fedha zaidi.
Hapa ni mawazo kumi ya kuingiza fedha kwa kutumia fedha.
- Kuwekeza fedha zako kwenye maeneo yanayozalisha faida.
-
Kufanya biashara ya kuwakopesha watu fedha kwa riba.
-
Kuwa mwekezaji wa mtaji kwenye biashara za watu wengine.
-
Kununua dhamana zinazouzwa kwa bei rahisi na kuziuza taratibu kwa bei nzuri. Hapa ni pale taasisi za kifedha zinapouza dhamana za wateja wao walioshindwa kulipa mikopo.
-
Kudhamini mashindano au matukio mbalimbali na kupata faida kwa njia mbalimbali.
-
Kufadhili mawazo mazuri ya kibiashara na kufaidika pale yanapofanya vizuri.
-
Kufadhili mawazo ya kibunifu na kunufaika pale yanapoleta matokeo mazuri.
-
Kuweka fedha kwenye akiba maalumu ya benki ambayo inatoa riba nzuri.
-
Kutumia fedha kama dhamana ya kupata fedha zaidi.
-
Kukopesha fedha kwa vikundi kitu ambacho marejesho yanaweza kuwa ya uhakika zaidi.
Unapokuwa na fedha za ziada, hakikisha unazitumia kuzalisha fedha zaidi na zaidi. Mawazo haya na mengine ya aina hiyo, yanaweza kuleta faida nzuri kwa fedha unayokuwa nayo.
Kocha.