Mawazo 10 ya kuingiza fedha bila kuwa na fedha.

Huwa kuna kauli kwamba unahitaji fedha ili kupata fedha. Ilikuwa sahihi kipindi cha nyuma, ila siyo sasa.
Unaweza kuingiza fedha hata kama huna fedha kabisa.

Hapa ni mawazo kumi unayoweza kufanyia kazi.

  1. Fanya kazi au vibarua ambapo kinachohitajika ni nguvu zako tu na siyo ujuzi wowote. Nguvu tayari unazo.

  2. Tumia uzoefu wako kuwasaidia watu kufanya mambo mbalimbali na ulipwe.

  3. Omba kazi ya mauzo ambapo unatumia ushawishi wako kuwafanya watu wanunue na ukalipwa kwa kamisheni.

  4. Fundisha kile unachojua kwa njia mbalimbali na ulipwe.

  5. Andika kitabu na kukiuza kwa nakala tete, huhitaji fedha ili kuchapa.

  6. Wasaidie watu kuendesha kurasa za mitandaoni na kulipwa.

  7. Kuwa dalali au wakala wa vitu mbalimbali.

  8. Uza vitu ulivyonavyo ambavyo huna matumizi navyo.

  9. Kushiriki mashindano mbalimbali yanayohitaji kipaji, nguvu, ujuzi au uzoefu ulionao.

  10. Kutangaza biashara za wengine kwa njia mbalimbali, hasa za mtandao au kuwasiliana na wateja na kukipwa.

Hata kama huna fedha, usijiambie huwezi kupata fedha.
Njia za kupata fedha bila hata ya kuwa na fedha ni nyingi, zitumie.

Kocha.