Mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia uzoefu.
Kila mmoja wetu kuna uzoefu ambao anao.
Kuna vitu ambavyo watu huja kwako kukuomba uwasaidie.
Hilo ndiyo eneo ambalo una uzoefu nalo.
Hapa kuna mawazo 10 ya kuingiza fedha kupitia uzoefu wowote ulionao.
- Kuwashauri wengine kuhusu eneo hilo na wakakulipa.
-
Kuwa na blogu ambayo unaandika kuhusu eneo hilo na kutengeneza wasomaji ambao watakulipa kwa njia mbalimbali.
-
Kuandika kitabu.
-
Kuandaa kozi ya mafunzo na kuuza kwa njia ya mtandao.
-
Kuendesha mafunzo kwa vitendo ambapo watu wanahudhuria na kulipia.
-
Kutumia mitandao ya kijamii kushirikisha uzoefu wako na kuingiza fedha kupitia matangazo.
-
Kuwaongoza watu katika kufanya maamuzi sahihi na wakakulipa.
-
Kutengeneza video za kushirikisha uzoefu wako na kuweka kwenye mtandao wa YouTube na kuingiza kipato kwa matangazo.
-
Kuwa mnenaji unayeshirikisha uzoefu wako kwa wengine na kulipwa.
-
Kuwa dalali kati ya wenye uhitaji na wasambazaji kwenye eneo ambalo una uzoefu nalo.
Usikubali uzoefu wowote ulionao ukae bure tu, ugeuze uwe njia ya kuingiza kipato.
Kocha.