2395; Tayari Una Taarifa Za Kutosha, Anza…

Kama kuna kitu unataka kuanza lakini unajiambia bado hujawa na taarifa za kutosha, jua unajidanganya tu.

Hakuna sehemu rahisi kujificha kama kwenye kukusanya taarifa zaidi na kufanya tafiti.

Kwa zama za mafuriko ya taarifa tunazoishi sasa, ni rahisi kuzama na kupotelea kwenye kutafuta taarifa zaidi.

Lakini taarifa hizo nyingi unazopata zinakuwa hazina tija, maana haziendani sana na kile unachotaka.

Unachopaswa ni kuanza, hata kama unaona hujawa tayari au kuna mambo hujajua, wewe anza.
Kadiri unavyofanya ndiyo unajua maeneo yapi muhimu ziadi na hata unapotafuta taarifa, unajua zipi za msingi.

Usiache kufanya kwa sababu unaona bado hujawa na taarifa za kutosha, taatifa ulizonazo mpaka sasa zinakutosha kuanza.
Anza na kadiri unavyokwenda utasukumwa kupata taarifa zilizo sahihi zaidi.

Una taarifa za kutosha mpaka sasa, anza kuzitumia na utapiga hatua kubwa.

Kocha.