Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya miongozo muhimu sana tunayoizingatia kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni afya.
Tunaamini afya ndiyo mtaji wa kwanza na muhimu kwa mafanikio yetu.
Tunajua bila ya afya bora huwezi kufanikiwa na hata ukifanikiwa hutayafurahia na kuyafaidi mafanikio.
Afya imegawanyika kwenye maeneo matatu, afya ya mwili, akili na roho.
Na inapokuja kwenye afya, kinga ni bora kuliko tiba.
Kwenye afya ya mwili, moja ya vitu vinavyoijenga, kuilinda na kuikinga ni mazoezi.
Ufanyaji wa mazoezi ya mwili unafaida nyingi mno kiafya.
Tafiti nyingi zinaonyesha ni kitu pekee chenye ufanisi mkubwa kiafya kuliko aina yoyote ile ya dawa.

Kwa kutambua umuhimu huu wa afya kwenye safari yetu ya mafanikio, tutakuwa na mazoezi ya pamoja kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Mazoezi haya yatafanyika siku ya pili ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambayo itakuwa jumapili ya tarehe 17/10/2021 jijini Dodoma.
Mazoezi hayo yatakuwa ni ya kutembea kwa umbali wa kilomita tatu kwa pamoja.
Hii itakuwa nafasi nzuri sana kwa washiriki wote wa semina kuwa pamoja na kunufaika kiafya kwa mazoezi huku pia wakikuza mitandao yao.
Nichukue nafasi hii kuwakaribisha wote kwenye mazoezi haya ya pamoja, ambayo yana manufaa makubwa.
Kwenye mazoezi haya tutavaa tisheti maalumu za KISIMA CHA MAARIFA, lakini nguo ya chini kila mtu atavaa ya kwake.
Ni tukio ambalo washiriki wote wa semina tutalifanya kwa pamoja na kila mtu atakwenda kwa mwendo anaoweza. Hatutashindana bali tutashirikiana kwenye hili.
Tisheti za kushiriki mazoezi haya zitatolewa na KISIMA CHA MAARIFA. Unachopaswa kufanya ni kutuma ukubwa wa tisheti unayovaa ili iweze kuandaliwa. Tuma ujumbe kwenda namba 0717 396 253, wenye majina yako na ukubwa wa tisheti kama ni Small, Medium, Large, Extra Large n.k.
Kama bado hujathibitisha kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 fanya hivyo sasa, tuma ujumbe wenye majina yako na namba ya simu pamoja na ukubwa ea tisheti unayovaa kwenda namba 0717 396 253

Kama bado hujapata taarifa za semina, pata hapa kwa ufupi.
Nini; Ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ambayo huwa inafanyika kila mwaka na kuwakutanisha wote wenye kiu ya mafanikio makubwa.
Lini; Semina ya mwaka huu 2021 itafanyika kwa siku mbili, tarehe 16 na 17 mwezi Oktoba mwaka 2021.
Wapi; Semina itafanyika jijini Dodoma, kwenye moja ya hoteli zilizopo kwenye jiji hilo.
Gharama; Gharama za kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku zote mbili, ambayo itagharamia mambo yote ya semina isipokuwa malazi ambayo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
Manufaa; Manufaa ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni mengi. Utajifunza jinsi ya kuiishi falsafa ya mafanikio. Misingi na mikakati ya kuelekea kwenye ubilionea. Shuhuda za wanamafanikio waliopiga hatua kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yao. Kukaa ana kwa ana na kocha na kujadili mpango wako wa mwaka wa mafanikio. Kujenga mfumo wa kuiendesha vizuri biashara yako. Kukuza mtandao wako wa mafanikio kwa kukutana na watu sahihi kwako. Na mengine mengi mazuri kwa ajili ya mafanikio yako.
Malipo; Njia za kulipa ada ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni hizi zifuatazo;
1. Tigo pesa; 0717396253
2. Mpesa; 0755953887
3. CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700
4. NMB BANK, AC NO. 40302535762
Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
Mwisho wa kulipa ada ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni tarehe 01/10/2021.
Hatua za kuchukua sasa hivi;
1. Thibitisha kushiriki SEMINA kama bado hujafanya hivyo, tuma majina yako na kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253.
2. Tuma ukubwa wa tisheti unayovaa ili upate tisheti ya kushiriki mazoezi ya pamoja.
3. Andaa mpango wako wa mwaka wa mafanikio 2021/2022 ambao utaujadili kwa pamoja na kocha na akusimamie katika kuutekeleza.
Karibu sana rafiki yangu, SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ndiyo sehemu ya kukutana pamoja na kuwasha moto unaotusukuma mwaka mzima.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz