
Richard Feynman aliwahi kusema jukumu letu la kwanza ni kutokujidanganya kwa sababu ni rahisi mno kujidanganya wenyewe.
Hakuna mtu rahisi kumdanganya kwenye maisha yako kama wewe mwenyewe.
Kwa vitu unavyotaka na hujapata, utatafuta kila sababu ya kukuridhisha, isipokuwa kuukabili ukweli.
Utaangalia nini umekosa au ugumu gani unakabiliana nao. Lakini hutaangalia nini hujafanya ambacho kipo ndani ya uwezo wako.
Kwa kila sababu unayojipa ya kushindwa kufanya, kuna kitu unaweza kufanya kuivuka sababu hiyo.
Kama huamini, angalia wengine ambao waliweza kufanya licha ya kuwa na sababu kama yako. Na wapo wengi mno.
Kama wengine wameweza wana nini na wewe ushindwe una nini?
Ukurasa wa kusoma ni siyo kweli; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/21/2394
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma