Mawazo 10 ya kuingiza fedha unapokuwa chini kabisa.
Kuna wakati mtu unakuwa unapitia magumu sana kwenye maisha na kuona kama kila kitu hakiwezekani.
Unaweza kukata tamaa na kuona huna cha kufanya.
Lakini usiruhusu hilo, yapo mengi ya kufanya.
Na kuna njia mbalimbali za kuingiza fedha pale unapokuwa chini kabisa.
- Fanya vibarua mbalimbali. Una nguvu na muda, vitumie kufanya chochote halali na ambacho watu wapo tayari kukulipa.
-
Fanya kazi ya mauzo kwa kampuni mbalimbali ambazo zinauza bidhaa zake moja kwa moja kwa wateja.
-
Tumia ujuzi na uzoefu wako kutafuta kazi ya kuajiriwa. Tumia kila ushawishi kupata kazi.
-
Anza biashara kwa kutumia ujuzi, uzoefu, nguvu na muda wako. Hivyo viwe ndiyo mtaji wako wa kuanzia.
-
Kuwa dalali pale unapoweza kuwaunganisha wenye uhitaji na wauzaji wa bidhaa au huduma mbalimbali.
-
Waombe watu wako wa karibu wakusaidie kifedha na uwe na mpango wa jinsi ya kuzitumia kuondoka pale ulipokwama.
-
Uza vile ulivyonavyo ambavyo kwa hali unayopitia huwezi kuvitumia. Unachohitaji ni kuvuka salama, utaweza kununua chochote ukishavuka.
-
Jifunze na wafundishe wengine yale unayojifunza kwa njia mbalimbali na waweze kukulipa.
-
Ungana na wengine ambao tayari kuna kitu wanafanya na wewe peleka ujuzi, uzoefu, nguvu na muda wako.
-
Shusha sana hadhi ya maisha yako ili kupunguza mno gharama za maisha. Kuendelea kushikilia hadhi uliyokuwa nayo mwanzo wakati mambo yako ni magumu ni kuzidi kujididimiza. Unachotaka ni kuvuka salama na siyo kumfurahisha yeyote.
Unapokuwa chini, ni mahali pa zuri kuanzia kwa sababu huna pengine pa kwenda zaidi ya juu. Lakini pia wengine wanapojua upo chini, wanakuwa hawana mategemeo makubwa kwako na hivyo hawakusumbui sana.
Tumia wakati unaokuwa chini kupambana kuvuka salama na kurudi juu.
Kocha.