
Mafanikio yana gharama kubwa. Na mafanikio yanapoambatana na umaarufu, yanakuwa na gharama kubwa zaidi.
Wengi kabla hawajafanikiwa hutamani sana wapate umaarufu kwani huamini mafanikio yanayoendana na umaarufu ndiyo mazuri.
Lakini wakishafanikiwa na kuwa maarufu ndiyo wanagundua jinsi hilo lilivyo mzigo mkubwa.
Unapofanikiwa na kuwa maarufu unakuwa lengo la mashambulizi kwa kila mwenye chuki, hasira na kushindwa kwenye maisha yake.
Jitahidi sana kwenye safari yako ya mafanikio, watu wajue kuhusu wewe lakini wasikujue wewe. Hilo litakupa amani kubwa ya moyo na uhuru wa kuyaishi maisha yako.
Ukishakuwa maarufu unakuwa huna tena maisha binafsi, inabidi uishi maigizo ili kuendelea kutunza umaarufu wako.
Ukurasa wa kusoma ni mambo ya kuzingatia unapokuwa kwenye kilele cha mafanikio; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/07/24/2397
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma