Mawazo 10 ya kuingiza fedha kwa kipaji.

Kipaji ni kile kitu ambacho kwako ni kama mchezo, lakini kwa wengine ni kazi ngumu.
Wewe unafanya bila kuchoka, wakati wengine wanachoka kabla hata hawajaanza kufanya.

Hakuna asiye na kipaji, ila kuna wengi wasiojua vipaji vyao.
Pambana ujue kipaji chako na kisha kitumie kuingiza fedha kwa njia hizi 10.

  1. Wafanyie watu kile ambacho wewe ni rahisi kwako kufanya ila kwao ni vigumu na wakulipe kwa kufanya.

  2. Wafundishe wengine kile ambacho unafanya kwa urahisi.

  3. Andika kitabu cha jinsi mtu anaweza kuendeleza kipaji kama ulichonacho wewe.

  4. Tafiti maarifa zaidi kwenye eneo lako la kipaji na washirikishe watu kwa njia mbalimbali.

  5. Andaa mpango wa kuibua vipaji vilivyo ndani ya watu na waweze kufanya makubwa. Hao unaowasaidia wanakulipa.

  6. Kuwatambua watu wenye vipaji na kuwasaidia wavitumie na kufanya makubwa, kisha wanakulipa kwa usimamizi wako wa karibu kwao.

  7. Tengeneza video za kutoa mafunzo ya kipaji na kuweka kwenye mtandao wa YouTube kisha kuingiza fedha kwa matangazo.

  8. Changanya kipaji chako na ujuzi mpya na kuwa mtu wa kipekee ambaye hakuna anayeweza kushindana na wewe.

  9. Jenga ubobezi zaidi kwenye kipaji chako na kupata fursa kubwa zaidi.

  10. Kuchanganya vipaji mbalimbali ulivyonavyo, pamoja na uzoefu ulionao na kuzidi kuwa tofauti.

Ukishajua kipaji chako, usikiache kilale, tumia kila fursa kuingiza fedha kwa kipaji hicho.

Kocha.