Maamuzi mengi unayofanya kwenye maisha yako yanakuwa siyo sahihi kwa sababu unayafanya kwa kuangalia vitu kwa nje pekee.

Usiwe mtu wa kufanya maamuzi kabla hujaangalia kitu kwa ndani, maana kwa kufanya hivyo ndiyo unaujua ukweli wenyewe.

Kwa kuangalia kwa nje huoni ukweli ambao upo ndani. Kwa nje kila kitu ni rahisi, lakini kwa ndani vitu ni vigumu na vina changamoto nyingi.

Angalia kwa ndani ili ufanye maamuzi sahihi.

Ukurasa wa kusoma ni unachoona na usichoona; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/02/2406

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma