Rafiki yangu mpendwa,
Pata picha umeenda kwenye kisima cha maji safi ili kuteka maji ya kunywa.
Unafika na kumkuta mtu amekaa pembeni ya kisima huku anasononeka.
Unamuuliza tatizo ni nini?
Anakujibu ana kiu kali.
Unashangazwa, kiu gani tena wakati maji yako hapo pembeni yake, tena ambayo ni safi?
Anakuambia hajui atawezaje kuyanywa.
Hapo lazima utashangaa sana,
Na utaona kabisa kuna kitu ambacho hakipo sawa kwa mtu huyo.
Rafiki, hivyo ndivyo pia ilivyo pale mtu anayetumia simu janja ya mkononi (smart phone) anapokuwa analalamika kwamba hana njia ya kuingiza kipato cha ziada kwenye maisha yake.
Kama ilivyo kisima cha maji ambacho kina fursa za mtu kukata kiu yake, simu ya mkononi pia ina fursa kwa kila mtu kuweza kuongeza kipato chake.
Najua unatumia simu ya mkononi ndiyo maana umeweza kusoma hapa.
Swali langu kwako ni hili, je huwa unaweza kuingiza kipato moja kwa moja kwa kutumia simu hiyo?
Kama jibu ni ndiyo basi uko vizuri na nitakushirikisha namna ya kufanya kwa ubora zaidi.
Na kama jibu ni hapana basi una bahati nzuri, maana leo unakwenda kujifunza jinsi ya kuweza kufanya hivyo.
Kama utajifunza leo na kuchukua hatua, kamwe hutokuja kulalamika tena kuhusu kipato.

Rafiki, kwenye kitabu kipya nilichotoa ambacho kinaitwa SIMU YANGU OFISI YANGU nimekushirikisha hatua kwa hatua na kwa mifano rahisi kabisa jinsi unavyoweza kuigeuza simu yako kuwa ofisi yako inayokuingizia kipato.
Kitabu hiki kinakufaa sana kama tayari unaingiza kipato kwa simu yako, kwani kitakusaidia kufanya kwa mfumo mzuri zaidi.
Kwa nilichojifunza kwa wengi, wanafanya hili kwa kubahatisha na siyo kwa mfumo unaoeleweka na unaowapa uhakika.
Kitabu hiki kinakufaa zaidi kama bado hujaweza kuingiza kipato kwa simu yako, kwani kinakwenda kugeuza kile kilicho ndani yako kuwa msingi wa wewe kuingiza kipato kwa kutumia simu yako.
Rafiki yangu mpendwa, tayari unayo simu, unachohitaji sasa ni kujenga mfumo nzuri na wa uhakika wa kuingiza kipato kupitia simu hiyo.
Pata leo kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kujenga mfumo huo.
Rafiki, hiki siyo kitabu cha kukosa kama unataka kuongeza kipato chako zaidi.
Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.
Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.
Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.
Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf
Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz