2408; Kila kitu ni rasilimali…
Moto mkali unapokuwa unawaka, chochote kitakachowekwa kwenye moto huo hugeuka kuwa nishati ya kuuchochea zaidi.
Hata ukimwaga maji kwenye moto ambao ni mkali, unakuwa kama ni mafuta, yanachochea zaidi moto huo.
Hivyo ndivyo unapaswa kuyafanya maisha yako kuwa, tumia kila unachopitia au kukutana nacho kama rasilimali muhimu kwako kupata unachotaka au kufika unakotaka kufika.
Unataka kazi fulani ya ndoto yako na huipati? Mbona hiyo ni rasilimali tosha? Anzisha biashara yako mwenyewe na tengeneza kazi ya ndoto yako.
Unataka kuanza biashara lakini huna mtaji? Tumia hiyo kama rasilimali na uanze biashara bila ya mtaji.
Kuna watu wanakupinga, kukukatalia na kukukatisha tamaa? Safi sana, tumia hiyo kama rasilimali, waonyeshe kwamba wamekosea sana kukukadiria vibaya.
Kushindwa, mateso, kudhalilishwa, kukatishwa tamaa na kuumia, zote hizo ni rasilimali unazoweza kutumia ukafika kule unakotaka.
Uzuri ni tayari unazo rasilimali hizo, kazi ni kwako kuzitumia.
Kocha.
好的👌🏻
LikeLike
😊
Inabidi uwe unatutafsiria.
LikeLike