Rafiki, yangu mpendwa,
Ipo kauli ya Kiswahili inayosema kila zama na kitabu chake.
Ikimaanisha kila zama zina mambo yake muhimu kuzingatia ili kufanikiwa.

Wakati binadamu tunagundua zana za mawe, walioweza kutengeneza zana hizo ndiyo walionufaika sana.

Zikaja zama za chuma, ambapo walioweza kuzalisha na kudhibiti zana za chuma ndiyo walitawala dunia.

Yakaja mapinduzi ya kilimo, ambapo waliomiliki mashamba makubwa na yenye rutuba nzuri ndiyo walihodhi uchumi.

Mapinguzi ya viwanda yalizalisha matajiri wakubwa, ambao walikuwa wamiliki wa viwanda vikubwa.

Sasa tupo kwenye zama za taarifa, zama ambazo wanaozalisha, kusambaza na kudhibiti taarifa ndiyo matajiri wakubwa wanaohodhi uchumi.

Ukiangalia makampuni makubwa duniani kwa sasa, mengi yana msingi wake kwenye taarifa.
Apple, Facebook, Google, Microsoft, Amazon na mengine, yanategemea taarifa kama nguzo yake kuu.

Ukiwaangalia matajiri wakubwa duniani kwa sasa, ni ambao biashara zao zimejengwa kwenye msingi wa taarifa.  Jeff Bezos, Bill Gates, Mark Zuckerberg, Elon Musk na wengine, wamechuma utajiri wao kwa msingi wa taarifa.

Na hapo ndipo ninapokushauri ujijenge pia, hilo ndiyo eneo la kuwahi viwanja kwenye zama hizi.

Kama ambavyo watu walikuwa wanakimbilia kumiliki mashamba makubwa enzi hizo,
Na kama ambavyo wengi walikimbilia kusoma ili kupata kazi za viwanda ambazo kwa sasa hazipo,
Ndivyo kila mtu anapaswa kuhangaika ili kuhakikisha anajijengea njia ya kuingiza kipato kwa kutumia taarifa.

Eneo ambalo kila mtu anapaswa kuwahi kushika kiwanja chake kwenye zama hizi ni mtandaoni.
Huko mtandaoni ndiko unapaswa kujenga makazi yako ambayo utayatumia kuingiza kipato zaidi.

Kwa kuwa tupo kwenye zama za taarifa, zama ambazo maarifa na taarifa ndiyo nyenzo kuu, njia ya uhakika ya kuingiza kipato sasa ni kuwa kwenye sekta hiyo ya maarifa na taarifa.

Swali ni je unawezaje kuwahi viwanja kwenye zama hizi?
Na jibu ni rahisi kabisa, jibu lipo ndani ya kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU.

Hiki ni kitabu ambacho kinakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kujenga makazi yako mtandaoni.

Kitabu kinaanza na msingi ambao ni ujasiriataarifa.

Kinajenga nguzo ambayo ni thamani.

Kinakamilisha nyumba ambayo ni blog.

Kinaeleza vijiwe ambavyo ni mitandao ya kijamii.

Kinajenga jumuia ambazo ni makundi maalumu.

Rafiki, huo siyo mwisho wa mtiririko huo wa kujenga makazi ya mtandaoni.

Muhimu ni umeshaipata picha, sasa kilichobaki ni wewe uchukue hatua ili uweze kuwahi kiwanja na kujenga makazi yako mtandaoni.

Hatua ya kuchukua sasa hivi ni kujipatia nakala yako ya kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU ambacho kinapatikana kwa nakala tete.

Rafiki, hiki siyo kitabu cha kukosa kama unataka kuongeza kipato chako zaidi.
Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.

Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.

Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.

Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf

Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz