
Hakuna ambaye hana rasilimali muhimu anazohitaji ili kufanikiwa.
Kila siku tunakutana na rasilimali ambazo tukizitumia vizuri tutapata matokeo bora sana.
Kila magumu, changamoto na majanga unayokutana nayo ni rasilimali. Kila unayekutana naye ni rasilimali. Na kila unachojifunza ni rasilimali.
Usijiambie huna rasilimali, bali jiulize umezitumiaje mpaka sasa hizo ambazo tayari unazo.
Hakuna anayeshindwa kwa sababu amekosa fursa au rasilimali, kila mtu anakutana na hivyo, ni namna anavyochagua kuvitumia.
Ukurasa wa kusoma ni kutumia vizuri rasilimali unazokutana nazo; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/04/2408
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma