Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya mapinduzi makubwa yaliyoletwa na zama hizi za taarifa tulizopo sasa ni kila mtu kupewa jukwaa.
Katika zama hizi kila mtu ni mwandishi, kila mtu ni msanii, kila mtu ni mchekeshaji na kila mtu ni mhamasishaji.
Na kama huamini hilo, nenda kwenye WhatsApp yako sehemu ya Status na angalia status zilizowekwa na wale ambao una namba zao.

Kwa sehemu kubwa ni jumbe nzuri nzuri, za kuelimisha, kuhamasisha na pia kuchekesha.
Siku moja nimewahi kufungua status ya mtu ameweka ujumbe unasema leo sina cha kuwahamasisha kama vipi wewe kata tamaa tu.
Ni ujumbe unaochekesha lakini pia unabeba maana kubwa, watu wanaweka kazi kubwa kuhakikisha wanaweka jumbe nzuri.
Huwa nasema kama hujisikii vizuri, ukifungua baadhi ya status za watu unaweza kupata matumaini. Kwa sababu wengi wanaweka jumbe zenye mafunzo, hamasa na kutoa matumaini.
Sasa hilo ni eneo moja tu, hujaenda kwenye mitandao ya kijamii, ambapo japo wengi wanaigiza, lakini wanaonyesha maisha kuwa mazuri na yanayotoa matumaini.
Hata kama ni matumaini hewa, ni afadhali kuliko kukosa matumaini kabisa.
Kila mtu ana jukwaa, swali ni je unaweza kutumia jukwaa lako kuingiza kipato?
Je unajua kwamba hizo status unazoweka kwenye WhatsApp yako zinaweza kujenga biashara nzuri na inayokuingizia kipato?
Je unajua hao followers unaohangaika kuwapata kwenye mitandao ya kijamii unaweza kuwageuza wakawa wateja wazuri wa bidhaa na huduma mbalimbali?
Je unajua namna ya kutunza kila unachoweka mtandaoni ili kisizolewe na mafuriko ya taarifa?
Leo unapata nafasi ya kupata majibu yote hayo na kuweza kugeuza uwepo wako wa mtandaoni kuwa biashara inayokuongizia kipato.
Majibu yote hayo na mengine mazuri yapo kwenye kitabu kipya nilichoandika, kinachoitwa SIMU YAKO OFISI YANGU.
Kitabu kinachokupa msingi sahihi wa kuweza kujenga na kutumia majukwaa ya mtandao wa intaneti kuingiza fedha na siyo tu kupoteza muda wako.
Rafiki, hiki siyo kitabu cha kukosa kama unataka kuongeza kipato chako zaidi.
Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.
Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.
Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; http://www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.
Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf
Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz