2411; Usiige Matumizi…

Hakuna kitu rahisi kuiga kwa watu kama matumizi.

Hicho ndiyo tunaona kwa nje na kujilinganisha nao kisha kukimbilia kuiga.

Unapaswa kujua kitu chochote unachonunua kinapaswa kutokana na mahitaji yako kweli na siyo kwa sababu umeona wengine wanacho.

Wala usinunue kitu kwa sababu unataka wengine wakuone na wewe una kitu hicho.

Kumbuka wajibu wako wa kwanza kwenye maisha siyo kuwaridhisha wengine, bali kuishi maisha ambayo ni bora kwako.

Tambua pia hata unapokazana kuwaridhisha wengine, hakuna anayehangaika sana na namna unaishi maisha yako.
Kila mtu amevurugwa na maisha yake, anahangaika nayo zaidi.

Kuiga matumizi ni kuingia kwenye shimo ambalo litakupoteza kabisa kwenye maisha yako.

Kama unataka kuiga kitu kwa watu, iga nidhamu ya kazi na fedha.
Jifunze kwa wale wenye bidhamu nzuri kwenye hayo na wewe ujijengee nidhamu hizo pia.

Nidhamu ni nguzo itakayokujenga katika mafanikio. Hicho ndiyo kitu cha kuiga kutoka kwa wengine ambacho kitakuwa na manufaa kwako.

Usiige kazi au biashara wanazofanya, bali iga nidhamu wakizonazo kwenye kazi na biashara zao.
Usiige jinsi wanavyopata au kutumia fedha zao, bali iga bidhamu zao katika kuweka akiba na kuwekeza.

Nidhamu ni nguzo, ikiwa nayo unajenga makubwa.

Kocha.