Rafiki yangu mpendwa,
Nianze kwa kutangaza maslahi yangu,
Naamini sana kwenye vitabu.

Naamini kila mtu anapaswa kusoma vitabu ili kuweza kupata maarifa ya kuyaboresha maisha yake.

Naamini kila mtu ni kitabu kinachotembea, kwa yale ambayo mtu amepitia kwenye maisha yake, ni funzo kubwa kwa wengine.

Naamini kila mtu anapaswa kutoa kitabu kilicho ndani yake, kila mtu anapaswa kuandika kitabu kuhusu maisha yake au kingine chochote anachoweza kuwashirikisha wengine na wakajifunza.

Lakini wengi wamekuwa hawapo tayari kuandika vitabu, siyo kwa sababu hawana cha kuandika, ila kwa sababu wanaona hawana cha kuandikia.

Wengi hujiona siyo wabobezi kwenye kutumia kompyuta ili kuweza kuandika vizuri.
Na hivyo hutumia hiyo kama sababu ya kutokuandika.

Rafiki, zama zimebadilika sana, sasa hivi unaweza kuandika kitabu mpaka kukikamilisha kwa kutumia simu yako ya mkononi pekee.

Najua tayari unayo simu ambayo utaitumia kusoma hapa, sasa ninachokuambia ni hapo kwenye mikono yako umeshika mtambo ambao unaweza kuutumia kuandika kitabu.

Huhitaji kitu kingine chochote cha ziada, hiyo simu yako tayari inatosha kabisa.

Swali unalojiuliza ni je hilo linawezekanaje?

Na hapo ndipo nilipo na habari njema kwako, kwani nimekuandalia majibu ya uhakika ambayo unaweza kuyafanyia kazi na kuandika kitabu chako kwa simu.

Kwenye kitabu kipya nilichoandika, kinachoitwa SIMU YANGU OFISI YANGU nimekuonyesha jinsi unavyoweza kuandika kitabu kwa simu yako.

Ndani ya kitabu hicho utajifunza makubwa mawili;
Moja ni utaijua app ya kutumia kuweza kuandika kitabu kwa kutumia simu yako.
Uzuri wa app hiyo ni hata ukipoteza simu yako, hupotezi kazi yako, kwani inakuwa imetunzwa mahali salama mtandaoni.

Mbili ni utaijua app ya kutengeneza ganda la kitabu (book cover) kwa kutumia simu yako mwenyewe. Hapo kwenye ganda ni sehemu nyingine ambayo watu hukwama, hupaswi kukwama tena, jifunze sasa hatua sahihi.

Rafiki, sioni unasubiri nini mpaka sasa usisome kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU ambacho ni mwongozo sahihi kwako kuitumia simu yako kwa manufaa ya kifedha na kupiga hatua zaidi.

Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.

Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.

Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; http://www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.

Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf

Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz