
Hufanani na wengine kwa chochote kile, hivyo mengi unayoiga kwao yanakupoteza kwa sababu hayaendani na wewe.
Ila kuna kitu kimoja ambacho ukikiiga kwa wengine kinakuwa na manufaa makubwa sana kwako.
Kitu hicho ni nidhamu. Kwa kila unayemuona amepiga hatua kuliko wewe, jua ni nidhamu zipi zimemwezesha kupiga hatua hizo, kisha jijengee nidhamu hizo.
Nidhamu ni nguzo muhimu sana kwenye mafanikio ya aina yoyote ile, pambana kujijengea nidhamu kwenye kazi, muda, fedha na maeneo yote muhimu kwenye maisha yako.
Ukurasa wa kusoma leo ni usiige matumizi; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/07/2411
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma