Rafiki yangu mpendwa,
Leo nakwenda kukueleza ukweli ambao utakuuma, lakini ambao utakusaidia sana.
Umekuwa unahangaika na njia mbalimbali za kuongeza kipato chako, wakati kila siku umekuwa unapoteza fedha kwa kutumia simu yako.
Ndiyo, hiyo simu unayosoma nayo hapa, imegeuka kuwa tanuru la kuchoma fedha zako.
Hivyo kama unataka kupata fedha zaidi, inabidi uanze kwa kudhibiti hiyo simu yako ili iache kunyonya fedha zako.

Kuna njia tatu ambazo simu yako imekuwa inapoteza fedha zako.
Moja ni fedha unazotumia kuweka muda wa maongezi na kununua vifurushi mbalimbali, hasa vya mtandao. Gharama za vifurushi hivyo zimekuwa ni kubwa.
Mbili ni muda mwingi unaotumia kwenye simu yako ambao unakuwa hauzalishi. Mfano muda unaopoteza kwa kuzurura kwenye mitandao ya kijamii ambayo haikuingizii chochote, ni muda ambao unashindwa kuutumia kwa mambo yenye tija.
Tatu ni fursa nzuri unazozipoteza, fursa za kuingiza kipato kwa simu yako ambazo unashindwa kuzitumia kwa ufasaha ili ziwe na manufaa.
Hebu fikiria ni muda kiasi gani unatumia simu yako kila siku na ni kiasi gani umepoteza mpaka sasa?
Kwa hakika ni kiasi kikubwa.
Rafiki, kama unavyonijua, huwa sikuonyeshi tatizo bila ya suluhisho lake.
Na katika hili la kupoteza fedha kwa simu yako, nimekuandalia suluhisho la uhakika ambalo litakusaidia sana.
Baada ya kuona kilio cha wengi kwenye eneo hili,
Na baada ya kuona wengi wakiomba ushauri wanawezaje kutumia simu zao kuingiza kipato.
Nimekaa chini na kuandika kila ninachofanya katika kuingiza kipato mtandaoni kwa kutumia simu.
Yaani nimeshirikisha uzoefu wangu binafsi wa namna nimekuwa nafanya tangu mwaka 2013 mpaka sasa.
Hayo yote yako kwenye kitabu kipya nilichoandika kinachoitwa SIMU YANGU OFISI YANGU.
Kitabu hiki kina mafunzo ya kina na ya hatua kwa hatua kukuwezesha kuigeuza hiyo simu unayotumia sasa kuwa njia ya kujiingizia kipato.
Unahitaji nini tena rafiki yangu, yaani hapa kuna njia ya kugeuza hasara kuwa faida. Kufanya kitu kinachopoteza fedha kiweze kuingiza fedha.
Huhitaji kusubiri tena, unachopaswa ni kuchukua hatua sasa ya kupata kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU na uweze kuleta mabadiliko kwako.
Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.
Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.
Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.
Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf
Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz