2412; Ubahili na Ufanisi…
Rasilimali zote muhimu huwa zina uhaba.
Mahitaji huwa ni makubwa kuliko upatikanaji.
Na hapo ndipo tofauti kati ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa inapozaliwa.
Wanaofanikiwa ni wale wanaoweza kutumia vizuri rasilimali muhimu zenye uhaba.
Watu hao wanajua siri kubwa mbili ambazo wanazitumia vyema; uhaba na ufanisi.
Kwenye uhaba wanajipanga kutumia chini ya kile kinachopatikana.
Hawajiachii na kutumia mpaka kumaliza.
Badala yake wanatumia chibi ya kile kinachopatikana.
Lakini pia hawakubali kutumia huko kidogo kuwe kikwazo au changamoto kwao.
Badala yake wanajijengea ufanisi mkubwa, wanatumia vizuri kile kichache kinachopatikana ili kuzalisha matokeo makubwa.
Ufanisi ni kuweza kuzalisha matokeo makubwa na bora kwa kutumia rasilimali kidogo zilizopo.
Bila ya kuwa na ufanisi, ni vigumu kuweza kufanya makubwa.
Jua yale muhimu kabisa na yenye tija na hayo ndiyo uyape kipaumbele kwenye rasilimali zenye uhaba ulizonazo.
Iwe ni fedha, muda, umakini wako au nguvu kazi.
Tumia chini ya kinachopatikana na kile unachotumia kitumie kwenye yale muhimu pekee.
Kocha.