2419; Kwa nini ukweli ni mgumu kufikiwa…
Ni vigumu kuufikia ukweli kwa sababu huwa haubembelezi.
Ukweli hauangalii mtu anataka kusikia au kuona nini, unabaki kuwa ukweli.
Ukweli hauna mbwe mbwe wala kelele, unasimama kwenye eneo sahihi.
Sisi binadamu tunapenda mbwembwe nyingi, tunapenda vitu vinavyotusisimua.
Hivyo tunahangaika na yale yasiyo kweli mpaka tuyapate maumivu ya kutosha ndiyo tunakuwa tayari kwa ajili ya ukweli.
Kama unataka kuufikia ukweli, achana na mbwembwe, acha kutafuta kile kinachokufurahisha na nenda kwenye uhalisia wa mambo.
Ukweli haujali kuhusu hisia ulizonazo, unaweza kuchagua kuhangaika na hisia zako mpaka pale zinapokuumiza vya kutosha ndiyo utakuwa tayari kwa ajili ya ukweli.
Kocha.