Kama kuna kitu unafanya na hufanikiwi, ila unaona wengine wanafanya kitu hicho hicho na wanafanikiwa, mnatofautiana kwenye vipaumbele.

Wale wanaofanikiwa kwenye kitu hicho wanakuwa wamekipa kipaumbele cha kwanza, kwa sababu wameyafanya maisha yao kukitegemea kitu hicho.

Wewe ambaye hufanikiwi kwenye kitu hicho hujakipa kipaumbele cha kwanza, kwa kuwa maisha yako hayakitegemei kitu hicho.

Kama unataka kupata msukumo mkubwa wa kufanya na kufanikiwa kwenye kitu, yafanye maisha yako kutegemea kwenye kitu hicho.

Inapokuja kwenye maisha, hatusubiri au kuchelewa, siyo tunafanya kila kinachowezekana, bali tunafanya kila kinachopaswa kufanyika.

Ukurasa wa kusoma ni kwa sababu maisha yako yanakitegemea; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/14/2418

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma