Uongo na uzushi huwa unasambaa kwa kasi kuliko ukweli. Hiyo ni kwa sababu uongo uba mbwembwe nyingi na unagusa hisia hivyo kusambaa kama moto.

Ukweli hauna mbwembwe wala hauchochei hisia. Hivyo kuwa makini sana na taarifa unazopokea, kama huwezi kuzithibitisha kama ni kweli au la, angalia kasi ambayo taarifa hizo zinasambaa.

Ukiona zinasambaa kwa kasi sana na zinasambazwa hata na wale wasiozielewa, jua hapo uwezekano mkubwa ni uongo.

Ili uweze kuwa huru lazima utafute na kujua ukweli.

Ukurasa wa kusoma ni kwa nini ukweli ni mgumu kufikiwa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/15/2419

#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma