Rafiki yangu mpendwa,
Hivi unajua unaweza kuingiza kipato kikubwa kupitia uandishi wa hadithi?
Leo unakwenda kujifunza jinsi hilo linavyowezekana na hatua za kuchukua ili uweze kulipwa kupitia hadithi unazoweza kutunga.

Karibu kwenye makala hii ya ushauri wa changamoto ambapo unajifunza jinsi ya kuvuka vikwazo unavyokabiliana navyo kwenye safari yako ya mafanikio.

Msomaji mwenzetu aliyeomba ushauri kwenye hili alikuwa na haya ya kusema.

“Mimi napenda kuandika story kwenye blog ili niweze kuelimisha watu lakini sijui pa kuanzia.” – Pascal B. M.

Ili kuweza kuelimisha watu na kulipwa kupitia hadithi, fuata hatua hizi muhimu.

Moja; jua inawezekana.

Hatua ya kwanza ni kujua kabisa kwamba inawezekana kuelimisha watu na hata kuingiza kipato kupitia uandishi wa hadithi.
Wapo watu watakaokuambia haiwezekani, tayari kuna wengine wanafanya hivyo na mengine mengi.
Lakini wewe usiwasikilize, jua inawezekana na hata kama wengi wanaandika, bado dunia haijasikia hadithi yako na ubunifu wako.
Jiambie kila mara inawezekana na dunia inahitaji sana kusikia sauti yako.

Mbili; chagua eneo unalotaka kuelimisha.

Umeanza na msingi mzuri, wa kutaka kuelimisha watu kupitia hadithi.
Sasa changua ni eneo lipi unalotaka kuelimisha na watu wa aina gani unaowalenga.
Maeneo ya kuelimisha ni mengi lakini huwezi kufanyia kazi yote. Chagua lile ulilobobea au unalosukumwa sana kulifuatilia na kulijua na jijenge kwenye eneo hilo.
Uzuri wa hadithi ni kwamba hakuna kikomo kwenye yale unayotaka kufundisha.
Lakini pia mafunzo yake yanaeleweka zaidi kwa sababu yanagusa hisia kabisa.

Tatu; jenga makazi yako mtandaoni.

Baada ya kuchagua eneo utakaloelimisha na watu unaowalenga, kinachofuata ni kujenga makazi yako mtandaoni.
Kwanza kabisa fungua blog yako, kitu ambacho ni rahisi na unaweza kukifanya hata kwa kutumia simu yako. Soma mpaka mwisho kujua wapi pa kujifunza jinsi ya kutengeneza blog yako.
Pili tengeneza kurasa za mitandao ya kijamii zinazoenda kwa jina la blog yako, ili kuwafikia wapenzi wa aina ya hadithi unazoshirikisha na wenye kuhitaji mafunzo unayoyatoa.
Tatu kuwa na kundi kwenye moja ya mitandao ya kijamii, hasa wasap ambapo utawaalika wale wanaopenda kujifunza zaidi na walio makini kweli.

Nne; jenga hadhira yako.

Baada ya kuwa na makazi yako mtandaoni, kinachofuata ni kujenga hadhira, kupata wafuasi wa hadithi unazoandaa.
Hapa unahitaji kufanya kazi kubwa mbili;
Ya kwanza ni uzalishaji; kuandaa hadithi bora kabisa, zenye mafunzo ambayo watu wanayahitaji na ambazo watu wanavutiwa kuzisoma bila ya kuchoka. Tambua watu kwa sasa hawana muda, kama kitu hakiwavutii kusoma watajiambia watasoma baadaye na hilo kwa maana nyingine ni hawatasoma kabisa.
Ya pili ni usambazaji; kuwa na mfumo mzuri wa masoko wa kukuwezesha kuwafikia wale unaowalenga. Kwanza utaanza kwa kuwashirikisha wale wote unaowajua wewe. Kisha utawaomba wale wanaofurahia hadithi zako wasambaze kwa wengine ili nao wajifunze. Tatu unaweza kulipia matangazo mtandaoni na ukawafikia wengi.
Ukifanya vizuri kazi ya kwanza, ya pili itakuwa rahisi kufanya.

Tano; ingiza kipato.

Baada ya kujenga hadhira inayoelewa hadithi zako na kujifunza, sasa unaweza kuingiza kipato.
Mpaka sasa ulikuwa unafanya kazi kubwa na nzuri ila unaitoa bure kabisa, lengo lilikuwa kujenga hadhira na kuwafanya watu wajue thamani uliyonayo.
Sasa unahitaji kuigeuza hadhira hiyo kuwa wateja wanaolipia.
Na zipo njia mbalimbali za kufanya hivyo;
1. Kuwa na mfululizo wa hadithi ambapo mtu anapaswa kulipia ndiyo aupate. Hapo unaweza kuwa na blog maalumu ya kulipia ndiyo mtu asome au kundi maalumu ambapo mtu akilipia ndiyo anaunganishwa na kupata hadithi hizo.

2. Kuandika kitabu cha hadithi na kukiuza kwa wafuasi wa kazi zako. Hapo unawaonyesha jinsi kilivyo na mafunzo yenye manufaa kwao ili washawishike kununua. Kitabu kinaweza kuwa nalala tete au cha kuchapwa.

3. Wafundishe wengine jinsi ya kuandika hadithi. Kupitia uandishi wako utajenga wafuasi na katika wafuasi hao kuna ambao watapenda kujifunza uandishi kama wako. Hivyo unaweza kuendesha darasa la uandishi wa hadithi na watu wakalipia ili kujifunza.

4. Kutangaza biashara za wengine kwenye hadhira yako. Kama umeweza kutengeneza hadhira kubwa inayofuatilia kazi zako, unaweza kutangaza biashara za wengine na wakakulipa kwa sababu unawawezesha kuwafikia wengi.

Njia za kulipwa ni nyingi, ila hizo unaweza kuanza nazo mara moja na ukaanza kunufaika na uandishi wako.

Sita; pata na ufuate mwongozo huu.

Kama kweli umedhamiria kuwa mwandishi wa hadithi, kuzitumia kuwaelimisha wengine na kujiingizia kipato basi unapaswa kuwa na mwongozo sahihi unaoufuata.
Mwongozo huo ni kitabu kinachoitwa SIMU YANGU OFISI YANGU, kitabu hiki kinakupa mafunzo kamili ya jinsi ya kuweza kuwa mjasiriataarifa na ukajiajiri kupitia simu yako.
Kitabu kina haya uliyojifunza hapa yakiwa yameelezewa kwa kina zaidi.
Na kwenye kitabu utajifunza kwa picha jinsi ya kufungua blog yako wewe mwenyewe.

Jipatie kitabu hiki leo kwa bei ya zawadi ya tsh elfu 5 (5,000/=). Thamani halisi ya kitabu hiki ni kubwa, lakini nataka sana wewe rafiki yangu usiwe na sababu ya kukikosa.
Lipia leo tsh elfu 5 tu, uweze kupata kitabu hiki.

Kitabu kipo kwa mfuno wa nakala tete na unaweza kutumiwa kwa email au kukipata kwenye app.
Kitumiwa kwa email tuma fedha yako kwenda namba 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu; SIMU YANGU OFISI YANGU na utatumiwa kitabu.

Kukipata kitabu kwenye app ya SOMA VITABU fungua; http://www.bit.ly/somavitabuapp kisha utakipata kitabu na kukilipia kwenye app na kuweza kukisoma.

Kupata sehemu ya kitabu ili kuanza kujifunza pakua bure hapa; https://somavitabu.co.tz/wp-content/uploads/2021/08/PREVIEW-SIMU-YANGU-OFISI-YANGU-.pdf

Karibu sana rafiki yangu upate kitabu hiki cha SIMU YANGU OFISI YANGU ili uweze kuingiza fedha kwa kutumia simu yako ya mkononi na mtandao wa intaneti.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz