
Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii, huwa tunajali sana wengine wanatuchukuliaje.
Hilo lilikuwa muhimu kipindi cha nyuma, ambapo tuliishi ndani ya kundi lisilozidi watu 150 wanaojuana.
Kama kikundi chako kidogo kingekukataa, huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yako.
Lakini sasa tunaishi ndani ya kundi kubwa la watu na hakuna mwenye muda wa kuhangaika na maisha ya kila mtu.
Hakuna anayejali sana kuhusu maisha yako kama unavyodhani, hivyo kuwa huru kuyaishi maisha yako kwa namna yenye maana kwako.
Ukurasa wa kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/08/29/2433
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma