Habari Mwanamafanikio?
Karibu usikilize kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo kwa juma hili kuna mambo makubwa matatu.
Moja ni mafanikio ni vita, KISIMA CHA MAARIFA ni jeshi na wewe ni mwanajeshi kwenye hii vita. Hapa utajifunza kwa ufupi sifa za wanajeshi wa Sparta na mambo muhimu ya kuzingatia kwenye jeshi hili la KISIMA.
Mbili ni uchambuzi wa kitabu kinachoitwa Musashi’s Dokkodo (The Way of Walking Alone) ambacho kina Amri 21 za maisha ya kishujaa. Katika amri hizo 21 kuna mengi sana ya kujifunza katika kuishi maisha ya kijeshi.
Tatu ni mahojiano na mwanamafanikio mwenzetu Godfrey Mbise ambaye ni mstaafu, aliyechagua kustaafu kwa hiari miaka mitatu kabla ya umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Kwenye mahojiano haya Mzee Mbise anatushirikisha mengi kuanzia maamuzi yake ya kustaafu kwa hiari na yale aliyofanyia kazi baada ya kustaafu. Anatushirikisha kuhusu ufugaji wa kuku, ufugaji wa samaki na kilimo cha mbogamboga.
Mwisho kabisa kuna mjadala wa pamoja wa wanamafanikio ambapo wanashirikisha yale waliyojifunza pamoja na kuuliza maswali mbalimbali.
Karibu usikilize kipindi hiki ili uweze kujifunza na kuchukua hatua kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Kocha.