#SheriaYaLeo (22/366); Tumia ukinzani na magumu.

Ufunguo wa mafanikio kwenye tasnia yoyote ile ni kujijengea ujuzi wa aina mbalimbali kisha kuchanganya ujuzi huo kwa namna ya kipekee.

Lakini mchakato wa kufanya hivyo unaweza kuwa mgumu, wenye maumivu na kukatishwa tamaa. Maana kadiri unavyokwenda unagundua ukomo na ukosefu wa ujuzi muhimu.

Watu wengi huwa wanajaribu kukimbia huo ugumu. Wanajaribu kujiweka kwenye maeneo ambayo hawatakutana na ukosoaji au kupingwa ili kupunguza nafasi yao ya kushindwa.

Wewe hupaswi kufanya hivyo, chagua kuukabili ugumu, ukomo na hata maumivu kama njia ya kujenga ujuzi wako na kuweza kulifikia kusudi lako.

Sheria ya leo; Yapokee magumu na changamoto unazopitia. Kumbuka wakati ambao ulishindwa, kudhalilika au kukosolewa. Nini ulikuwa unafanya katika wakati huo na uzoefu huo umekufundisha nini?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#Ubunifu