#SheriaYaLeo (50/366); Chagua muda.
Chochote unachochagua kubobea, unahitaji muda wa kutosha kuweka juhudi ili kuweza kupata matokeo makubwa.
Kama una majukumu mengine mengi yanayochukua muda wako mwingi na kukuchosha, itakuwa vigumu kwako kifikia ubobezi unaotaka.
Kile unachotaka kubobea kinapaswa kuwa ndiyo kipaumbele kikubwa kwako, hivyo kitengee muda wa kutosha.
Yarahisishe maisha yako kwa kupunguza mambo unayojihusisha nayo kwenye siku yako.
Achana na yale yote ambayo hayana umuhimu mkubwa.
Kama inakubidi uwe na kazi nyingine ya pembeni ili kuwa na kipato cha kuendesha maisha, chagua kazi ambayo itakupa muda mwingi zaidi hata kama malipo yake yatakuwa kidogo.
Muda ni rasilimali muhimu kwako kufika kwenye ubobezi unaotaka, utenge wa kutosha na ulinde usipotee kwenye mambo yasiyo muhimu.
Sheria ya leo; Muda ni muhimu, punguza kitu kimoja kwenye siku yako leo ili upate muda zaidi wa kuweka kwenye ubobezi wako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu