#SheriaYaLeo (58/366); Anzisha Mtindo wako mwenyewe.

Wakati unaanza kujifunza kutoka kwa wengine, unawaiga na kufanya kama wao.
Hilo ni muhimu kwenye kujifunza na kuijua misingi muhimu ya kile ulichochagua.
Lakini kama utaendelea hivyo kwa wakati wote, hutaweza kufikia ubobezi wa hali ya juu.

Ili kufikia ubobezi wa hali ya juu, lazima uanzishe mtindo wako mwenyewe.
Ni lazima uonyeshe tofauti na upekee wako wewe na wengine.

Ni kupitia kuanzisha mtindo wako mwenyewe ndiyo unajitofautisha na wengine na kuweza kuzalisha matokeo ya kipekee, kitu kinachokufikisha kwenye ubobezi wa hali ya juu.

Sheria ya leo; Fuata mifano ya waliobobea lakini siyo njia zao. Onyesha utofauti wako kwa kuanzisha mtindo wako mwenyewe.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu