Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye msimu huu wa sikukuu, umeombwa na kutoa zawadi mbalimbali kwa watu wengi wa karibu kwako.

Umekuwa tayari kufanya hivyo kwa sababu ni watu muhimu sana kwako, watu ambao unawajali sana na umetaka kuona wakifurahia msimu huu wa sikukuu.

Lakini kuna mtu mmoja muhimu zaidi kwako ambaye umemsahau katika kumpa zawadi.
Mtu huyo ni wewe mwenyewe.

Unaweza kuwa umejipa zawadi ya nguo, sherehe na mengine ya aina hiyo.
Lakini hizo ni zawadi za kupita, ambazo muda mchache utakuwa umezisahau kabisa.

Kwa kuwa wewe ni rafiki yangu na ninakujali sana, kuna zawadi moja kubwa sana ninayokwenda kukushauri ujipe wewe mwenyewe kwa mwaka mpya wa 2022.

Zawadi hiyo ni KUANZA BIASHARA kama bado hujaanza na kama tayari umeshaanza basi ikuze biashara yako mara mbili ya ilivyo sasa.

Kama bado hujaanza biashara najua kwa muda mrefu umekuwa unajiambia utaanza ila unaona hujawa tayari.
Umekuwa unasubiri mpaka kila kitu kikamilike ndiyo uanze.
Na hapo ndipo umekuwa unajichelewesha wewe mwenyewe.

Leo nakuambia upo tayari kuanza biashara.
Tayari unacho kila unachohitaji ili uweze kuanza biashara yako.
Ni wewe tu kuamua kuanza na kuanza mara moja.
Na hapa nimekuandalia zawadi ambayo itakuwezesha ukamilishe hilo.

Kama tayari una biashara, najua umekuwa unaiendesha kwa mazoea kwa muda sasa.
Umeridhika na wateja ambao tayari unao na kiasi cha mauzo unayofanya.

Lakini kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho ni biashara yako bado ina nafasi ya kukua zaidi.
Unaweza kuongeza wateja zaidi na kuongeza mauzo zaidi.
Hivyo zawadi ya kujipa 2022 ni kuongeza wateja mara 2 ya ulionao sasa na kuongeza mauzo yako mara mbili pia.

Usijiambie hilo ni gumu au haliwezekani, kwani nimekuandalia zawadi ya kuhakikisha linawezekana kabisa kwako.

Hivyo rafiki yangu, jipe zawadi ya kuanza biashara kama bado hujawa na biashara na kama tayari unayo biashara, ikuze mara mbili ya ilivyo sasa.

Zawadi ya kukuwezesha kukamilisha zawadi yako.

Rafiki yangu, kwa sababu nakupenda na kukujali sana, nimekuandalia zawadi nzuri itakayokuwezesha kukamilisha kujipa zawadi ya biashara.

Zawadi hiyo ni kupata vitabu vinne muhimu sana ambavyo vitakuwezesha kukamilisha lengo hilo la zawadi yako binafsi.

Kitabu cha kwanza ni ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA. Hiki kitakuwezesha kujua mambo yote ya msingi ya kuzingatia kwenye biashara.
Kitabu hiki kinauzwa tsh elfu 20.

Kitabu cha pili ni BIASHARA NDANI YA AJIRA. Hiki kitakupa mawazo ya biashara unazoweza kuanza nazo, kuanzia biashara isiyohitaji mtaji kabisa, ya mtaji kidogo na kuendelea.
Kitabu hiki kinauzwa tsh elfu 20.

Kitabu cha tatu ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Hiki kitakuwezesha kujijengea nidhamu ya fedha ambayo ni muhimu sana kwenye kuanzisha na kukuza biashara yako.
Kitabu hiki kinauzwa tsh elfu 20.

Kitaby cha nne ni UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.  Hiki ni kitabu kinachokuonyesha nguvu kubwa iliyopo ndani yako na jinsi ya kuitumia kufanya makubwa.
Kitabu hiki kinauzwa tsh elfu 20.

Ila habari njema kabisa na zawadi ambayo nimekuandalia wewe rafiki yangu ni hii; ukinunua vitabu vitatu kati ya hivyo vinne, kimoja utapata bure kabisa.
Ndiyo rafiki, leo nakupa zawadi ya kitabu hicho cha bure ili kuhakikisha unakwenda kuanza au kukuza biashara yako mwaka 2022.
Kupata zawadi hiyo ni wewe kuchukua hatua ya kununua vitabu vitatu na upate kimoja bure.

Zawadi kuubwa zaidii…

Kama hiyo haitoshi, nimekuandalia zawadi nyingine kubwa zaidi ambayo ni mazungumzo kwa njia ya simu kwa muda wa saa moja.
Baada ya kununua vitabu hivyo na kuanza kwa kusoma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, nakupa nafasi ya kufanya mazungumzo ni mimi rafiki na Kocha wako.
Kwenye mazungumzo hayo utanishirikisha wazo la biashara ulilochagua au mikakati yako ya ukuaji kisha tutajadili kwa kina namna unavyokwenda kutekeleza hayo.

Rafiki, hiyo ni nafasi ya kipekee kabisa ambayo huwa haipatikani kirahisi.
Kutokana na mambo mengi yanayonikabili, huwa sipati nafasi ya kufanya mazungumzo na kila mtu, hata ambao wapo tayari kulipia.
Lakini wewe unakwenda kuipata nafasi hii bure kabisa kwa kuchukua hatua ya kununua vitabu vitatu leo hii.

Kupata zawadi hizi, wasiliana sasa na namba 0752 977 170, lipia vitabu vyako vitatu na upate vinne.
Anza kusoma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, chagua wazo utakalofanyia kazi, kisha wasiliana na mimi moja kwa moja kwa namba 0717 396 253 ili tupange kuwa na mazungumzo.

Rafiki, zawadi hii ya kipekee kabisa kwako ni kwa siku ya leo pekee, hivyo chukua hatua sasa kuwasiliana na 0752 977 170, upate vitabu vyako na kujiwekea nafasi ya mazungumzo na Kocha.

Kama tayari umeshakuwa na vitabu hivyo au baadhi ya hivyo vitabu, unaweza kumnunulia mtu wako wa karibu kama zawadi halafu wewe ukapata fursa ya kipekee ya mazungumzo na kocha.
Cha kufanya wasiliana na namba 0752 977 170 sasa, lipia vitabu vitatu ili upate vinne halafu wasiliana nami kwa namba 0717 396 253 tupange mazungumzo.

Mwaka 2022 utakuwa bora kwako kulingana na hatua utakazokwenda kuchukua.
Moja ya hatua muhimu ni kuanzisha biashara kama huna au kukuza biashara ambayo tayari unayo.
Hiyo ndiyo zawadi bora kabisa unayoweza kujipa.
Changamkia sasa zawadi niliyokupa hapa ili mwaka 2022 uende kuwa wa tofauti kabisa kwako.
Wasiliana na 0752 977 170 sasa.

Rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.